RUWASA PWANI YAWAONDOLEA KERO YA MAJI SAFI NA SALAMA WANANCHI ZAIDI YA ELFU 10 WILAYA YA MKURANGA

Naibu waziri wa maji Mhandisi MaryPrisca Mahundi wa kushoto akiwa amebeba ndoo ya maji kwa ajili ya kumtwisha kichwani mmoja wa wakinamama katika kijiji cha Mkerezange ikiwa ni ziara yake ya kikiza katika mradi huo wa matazamio.



Mmoja wa wakandarasi wa baadhi ya miradi iliyopo katika halmashauri ya Mkuranga Mkoa wa Pwani akiwa naye anamtwisha ndoo ya maji mmoja wa wakinamama waliohudhulia katika ziara hiyo ya kujionea mradi wa matazamio.



Naibu waziri wa maji Mhandisi Mary Prisca wa kati kati akiwa ameambatana na viongozi wa serikali ambapo kushoto kwake ni mkuu wa Wilaya ya Mkuranga na kulia kwake ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Pwani wakiangalia na kugagua moja ya miundombinu ya mradi wa maji ambao unatekelezwa.



Naibu Waziri wa maji Mhandisi MaryPisca Mahundi wa kati kati akiwa anazungumza jambo na mmoja wa wakinamama wa kijiji cha mkerezange kata ya Mkamba wakati wa ziara yake ya kikazi ya kwenda kugagua na kutembelea miradi mbali mbali ya wa maji inayotekelezwa Ruwasa katika halmashauri ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Kadija Ally.



Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mkuranga wa kushoto Injinia Maria Malala akimpatia maelezo Naibu waziri wa maji MaryPrisca Mahundi wa kati kataka kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbali mbali katika Wilaya ya Mkuranga.



WANANCHI zaidi ya elfu 10 kutoka kata mbili za Mwanambaya pamoja na kata ya Mkamba zilizopo katika halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya kutembea umbari mrefu hususan wakinamama kwa ajili ya kusaka maji usiku na mchana hatimaye wamepata mkombozi baada ya kukamilika kwa miradi miwili ya maji safi na salama.

Hayo yamebainika wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri wa maji Mhandisi MaryPisca Mahundi yenye lengo la kutembelea na kufanya ukaguzi wa miradi mbali mbali ambayo inatekelezwa katika Wilaya ya Mkuranga na Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira (RUWASA) Mkoa wa Pwani.

Katika ziara yake hiyo Naibu Waziri amebainisha kwamba lengo kubwa la serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kwamba inaboresha miundombinu ya upatikanaji wa maji safi na salama na kuwasadia wananchi wote hasa wakinamama kuwatua ndoo kichwani pamoja kuondoka na kero ya kutembea umbari mrefu.

“Nipo katika ziara yangu ya kikazi katika baadhi ya wilaya za Mkoa wa Pwani na leo nimefanya ziara katika Wilaya ya Mkuranga na kwa kweli nimeweza kujionea miradi miwili mikubwa ya maji ambayo inasimamiwa na wenzetu wa Ruwasa lakini kitu kikubwa nina imani kwamba wanawake wa maeneo hayo wataweza kuondokana na changamoto ya kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda kuchota maji ya kisima,”alisema Naibu Waziri.

Pia aliwataka wananchi wote wa Wilaya ya mkuranga kutoa sapoti na ushirikiano wa kutosha kwa wakandarasi ambao wanajenga miradi hiyo pamoja na kuhakikisha kwamba wanailinda miundombinu ya maji isiweze kuharibiwa na wala kuibiwa na badala yake waitunze ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu bila ya kuwa na mapungufu.

Kadhalika aliwapongeza uongozi wa Ruwasa Mkoa wa Pwani na kuwataka waendelee zaidi ya kufikisha huduma ya maji safi na salama katika maeneo mengine ambayo yamekuwa na changamoto kubwa ya wananchi kutokupata huduma hiyo na kuongeza kwamba serikali itaendelea kuweka mipango madhubuti yenye lengo la kutatua kero za maji kwa wananchi wake.

Katika hatua nyingine aliwataka wakandarasi wote kuhakikisha kwamba wanatekeelza majukumu yao ipasavyo na kumaliza miradi ambayo wamepangiwa kwa wakati ili kuweza kuwapa fursa wananchi waweze kuanza kuitumia miradi hiyo kwa muda ambao umepangwa na kuahidi kuyafuatilia malipo yote ambayo yanadaiwa na baadhi ya wakandarasi.

Naye Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Mkuranga Injinia Maria Malala amebainisha kwamba kwa sasa kiwango cha upatikanaji wa maji ni aslimia 76 na kwamba na kwamba wanatarajia kufikisha huduma hiyo kwa wananchi mbali mbali kutoka kata zipatazo 19 wanazozihudumia.

Kadhalika alioongeza kuwa katika mwaka wa fedha wa kuanzia 2021 /2022 Ofisi ya Ruwasa Wilaya ya Mkuranga inaendelea na utekelezaji wa miradi ipatayo sita,ambayo itatumia mfuko wa maji wa (NWF) na kwamba utekelezaji wake utakusa katika maeneo mbali mbali yakiwemo Mwanambaya,Mkerezange,Msorwa,Mvuleni Kilimahewa kusini, pamoja na ujenzi wa mradi wa kijiji cha Mdimin ambao utakamilika octoba 2021.

Nao baadhi ya wakinamama wanaoishi katika kaya ya Mwanambaya akiwemo pili Rajabu wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kushirikiana na uongozi wa Ruwasa kwa kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa maradi huo ambao kwa upande wao utakuwa ni mkombozi mkubwa sana.

Alifafanua kuwa cha kipindi cha miaka mingi wakinamama hao walikuwa wanakabili na baadhi yao ndoa za kuvunjika na kuachwa na wanaume zao kutokana kutumia muda mwingi wakiwa visimani kwa ajili ya kuchota maji umbari mrefu na kupelekea kuchelewa kurudi majumbani kwao kwa wakati hivyo wakati mwingine wanajikuta wanapata kipigo.

WAKALA wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Pwani kwa sasa inahudumia katika maeneo mbali mbali ya Wilaya hiyo ya Mkuranga ambapo jumla ya kata 19 na kwamba imefanikiwa kutekeleza mradi mkubwa wa kusambaza maji safi na salama awamu ya kwanza uliofadhiliwa na Dawasa kwa Gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 5.5.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post