KIJIJI CHA NAMINYWILI-RUFIJI KUONDOKANA NA KERO YA MAJI ILIYODUMU KWA KIPINDI KIREFU-LT MWAMBASHI

KIONGOZI wa mbio za mwenge maalum wa uhuru, LT.Josephine Mwambashi amekemea vitendo vya baadhi ya watu wanaoharibu miundombinu ya maji ,ambapo ameiasa jamii kulinda na kutunza vyanzo na miundombinu ya miradi ya maji.

Akizindua mradi wa maji Kijiji cha Nyaminywili , Rufiji mkoani Pwani,unaosimamiwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) na kukamilika kwa asilimia 100 kwa gharama ya milioni 195.358.2, Mwambashi alisema, maji ni uhai yapaswa kulinda miundombinu yake kwa manufaa ya jamii.

Alisema, serikali ya awamu sita ,inayoongozwa na Rais Samia Suluhu inajitahidi ili kila mwananchi afikiwe na huduma muhimu ikiwemo maji.

Mwambashi alifafanua, serikali imejipanga kwa kutenga fedha kutekeleza miradi ya maji ,mijini na vijijini ili kuondoa tatizo sugu la maji kwa kumtua ndoo mama kichwani.

"Wasimamizi wa miradi hii inapaswa nanyi muwe wazalendo na kuwashirikisha wananchi katika hatua za utekelezaji"alibainisha Mwambashi.

Hata hivyo , Mwambashi alielekeza RUWASA kuandaa taarifa ya kiasi cha sh.milioni mbili ambazo hazijawekwa katika taarifa ya mradi huo .

Awali akielezea,mradi huo ,meneja wa RUWASA Rufiji,Tluway Ninga alisema, makisio ya mradi huo yalikuwa milioni 257.543.3 , utekelezaji ulianza julai 2020 na kukamilika julai 2021.

Ninga alisema kuwa, mradi huo unasaidia wakazi 2,573 wa Nyaminywili kwa kupata huduma ya maji safi na salama na kuondokana na kero hiyo sugu iliyodumu kwa miaka takriban 30.

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post