Katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi Anthony sanga amezindua
miongozo mitatu inayolenga kuwezesha na kurahisisha utendaji kazi katika
mamlaka za maji nchini. Miongozo hiyo ni muongozo wa kuandaa mkakati wa
kupunguza upotevu wa maji , muongozo wa usimamizi wa Dira za maji na muongozo
wa uendeshaji wa mamlaka za maji.
Katika hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na mamlaka ya udhibiti
wa huduma za Nishati na maji (EWURA) jijini
Dar es salaam.
Amesema Rais ameonyesha nia ya dhati ya kutatua changamoto
za upatikanaji wa huduma ya maji kwa watanzania hivyo watumishi wa wizara wana
jukumu la kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao.
Aidha katika hafla hiyo mhandisi sanga amekabidhi zawadi za
vyeti na ngao kwa mamlaka za maji ambazo zimefanya vizuri katika utekelezaji wa
majukumu yao katika maeneo tofauti tofauti.
Vilevile amewapongeza EWURA kwa kuweka utaratibu wa kutoa zawadi mamlaka za maji ambazo zimefanya kazi nzuri katika utekelezaji wa majukumu yao.