Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amezungumza na wananchi wa kijiji cha Mahege wilayani Kibiti mkoa wa Pwani.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amezungumza na wananchi wa kijiji cha Mahege wilayani Kibiti mkoa wa Pwani. Amewahakikishia kuwa Serikali iko tayari kutekeleza mradi wa maji katika eneo hilo ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa majisafi.




Amesema mwezi wa 8 Serikali italeta milioni 100 ili kuanza kutekeleza mradi huo ambao RUWASA wilaya wamesanifu na kubaini kuwa utagharimu shilingi milioni 600.

"Niwahakikishie kuwa mradi huo utatekelezwa mapema iwezekavyo. Wataalam wangu wameniambia utachukua miezi sita kukamilika, hivyo msiwe na wasiwasi. Rais Samia amejipambanua kuwa 'mama maji.' Hataki kuona akina mama wa kitanzania wakihangaika kupata huduma ya majisafi na salama." Amesema Mhandisi Mahundi.







Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post