Kaimu Meneja wa Mkoa, Eng. Eva Kahwili alisema lengo kuu la
kikao hiki ni kutambulisha ujenzi wa Mradi wa Maji Kwala na pia kumtambulisha
Mkandarasi ambaye ni JECC’s.
Pia, alisema kuwa Mradi huu utagharimu kiasi cha shilingi za
Kitanzania bilioni 1.4 na itakuwa na
vituo 12 ambapo Kijiji cha Kwala kitakuwa na vituo 9 na Kijiji cha Mwembe ngozi
vituo 3 na utatekelezwa ndani ya miezi sita.
Pia, kutakuwepo na tenki la maji lenye ujazo wa lita 500,000
ambalo litakuwa linasambaza maji katika vijiji hivyo.
Pia, Kaimu Meneja wa Mkoa Eng. Kahwili alimuomba Mkandarasi
aweze kushirikiana na wanakijiji wa Kwala na Mwembe Ngozi hususani katika ajira
ndogo ndogo katika kipindi chote cha utekelezaji wa Mradi huo.
Pia, aliwataka wanakijiji waweze kulinda mali za Mradi kwani
Mradi huu ni Mradi wa wanakijiji wote, hivyo wizi wa namna moja au nyingine
utasababisha ucheleweshaji wa Mradi.